Sherehe hii ilihitimishwa kwa hali ya kiroho, upendo na nuru, na kwa mara nyingine tena, nyoyo za wapenzi wa Mtume wa Rehema (s.a.w.w) na Imam as-Sadiq (a.s) ziliunganishwa pamoja. Tunatarajia kwamba sherehe kama hizi ziendelee kuwa chachu ya kuimarisha imani, mshikamano na hamasa ya elimu katika jamii ya Kiislamu.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Taasisi ya Jamiat Al-Mustafa (s) - Tawi la Malawi - Kwa mnasaba wa kuwadia siku tukufu za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad Al-Mustafa (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Ahlul-Bayt wake) pamoja na Imam Ja‘far as-Sadiq (a.s), sherehe yenye heshima, baraka na upekee ilifanyika kwa kuhudhuriwa na Waumini Wapenzi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kutoka maeneo mbalimbali, wakiwemo Wasomi na Maulamaa, wanafunzi na wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s). Sherehe hii iliandamana na mazingira ya kiroho na hamasa kubwa kutoka kwa washiriki.
Ufuatao ni Muhtasari wa Vipengele vya Sherehe Hii
1. Usomaji wa Qur’an Tukufu
Sherehe ilianza kwa tilawa ya maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu Qur’ani Tukufu, iliyosomwa na Qari mashuhuri Sheikh Abdurashid Yusuf. Sauti yake ya kuvutia ilijaza ukumbi kwa nuru ya aya za Mwenyezi Mungu.
2. Wimbo wa Taifa
Baada ya Qur’an, washiriki walisimama kwa heshima na kuimba Wimbo wa Taifa la Malawi, jambo lililotangaza ufunguzi rasmi wa sherehe hiyo.
3. Hotuba ya Makaribisho
Sheikh Abdurashid Shuaib aliwakaribisha wageni wote kwa maneno ya upendo na mshikamano, akieleza umuhimu wa kuadhimisha siku hizi tukufu na akawashukuru Maulamaa na wanafunzi kwa mahudhurio yao makubwa.
4. Ushairi
Wanafunzi wawili, ndugu Amini na Umar, walisoma mashairi yenye maudhui ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w). Ushairi wao mzuri uliamsha hisia na kupata sifa kutoka kwa washiriki.
5. Mada: Uumbaji wa Nuru ya Mtume (s.a.w.w)
Sheikh Nuruddin Biyisa alitoa maelezo ya kina ya kielimu na kiroho kuhusu mada ya Uumbaji wa Nuru ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), akiegemea katika Aya na Riwaya za Kiislamu.
6. Mada: Enzi ya Jahiliyya
Wanafunzi wawili, ndugu Rasuli Was na Hanafiy Mutawalla, walitoa hotuba kuhusu hali ngumu za kijamii, kimaadili na kiutamaduni zilizokuwepo wakati wa kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w) katika zama za jahiliyya.
7. Nashidi kuhusu Kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w)
Kikundi cha wanafunzi waliimba nashidi yenye mvuto kuhusu kuzaliwa kwa Mtume wa Rehema (s.a.w.w), hali iliyoongeza msisimko na furaha katika ukumbi.
8. Mada: Mapenzi kwa Mtume (s.a.w.w)
Sheikh Bashir Ajsa alizungumzia mada ya Mapenzi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), akieleza nafasi ya upendo kwa Mtume katika malezi ya kiakhlaqi na kidini ya jamii ya Kiislamu.
9. Hotuba ya Mwisho
Ustadhi Azhar alihitimisha sherehe kwa kusisitiza juu ya fadhila za umoja wa Kiislamu, ufuatano wa maadili na mwenendo wa Mtume (s.a.w.w), pamoja na umuhimu wa kutafuta elimu.
10. Tuzo kwa Wanafunzi Bora
Wanafunzi walioonesha juhudi na mafanikio bora katika masomo, maadili na tablighi walituzwa zawadi maalum. Tukio hili liliwatia moyo wanafunzi wote na kuongeza hamasa ya kujitahidi zaidi.
11. Hotuba ya Shukrani
Mmoja wa waandaaji wa sherehe alitoa maneno ya shukrani kwa walimu, wanafunzi, wageni na wote waliosaidia katika maandalizi ya hafla hii.
Sherehe hii ilihitimishwa kwa hali ya kiroho, upendo na nuru, na kwa mara nyingine tena, nyoyo za wapenzi wa Mtume wa Rehema (s.a.w.w) na Imam as-Sadiq (a.s) ziliunganishwa pamoja. Tunatarajia kwamba sherehe kama hizi ziendelee kuwa chachu ya kuimarisha imani, mshikamano na hamasa ya elimu katika jamii ya Kiislamu.
Tumekuwekea picha zaidi za tukio hapo chini
Your Comment